Your Cart
Loading

Kutoka Kusuasua Hadi Kupaa: Mbinu 6 za Darasani Zinazowasaidia Wanafunzi Wanaosuasua Kufikia Mafanikio Makubwa

On Sale
$5.00
$5.00
Added to cart

Kila darasa lina wanafunzi wachache walio nyuma. Hawanyooshi mikono. Madaftari yao yanarudi yakiwa mekundu kwa alama za kosa. Na taratibu wanaanza kuamini kwamba wao ni "wazito" au "hawana akili".

Si kweli. Wengi wao wamepitwa na mada za madarasa ya nyuma. Wengine wamechoka, wengine wanaogopa kuchekwa, na wengine hawajapata mtu wa kuwaonyesha njia.

Mwongozo huu, Kutoka Kusuasua Hadi Kupaa, una mbinu sita rahisi za kubadili hali hiyo. Hazihitaji kompyuta wala darasa dogo. Zinafanya kazi kwenye madarasa yetu halisi, hata darasa la wanafunzi 60 hadi 80 lenye ubao mmoja.

Ndani utapata:

  • Mbinu 1: Wanafunzi wasaidiane, wasishindane. Darasa zima liwe timu moja, na lipande pamoja.
  • Mbinu 2: Anza somo kwa maswali. Anza na mambo wanayoyajua tayari, kisha panda kidogo kidogo hadi somo jipya.
  • Mbinu 3: Fundisha kwa michezo. Michezo saba isiyo na gharama, kama kupanga safari ya kupanda Kilimanjaro na siku ya soko.
  • Mbinu 4: Pima uelewa mara kwa mara, msifu kila anayejaribu. Njia za haraka za kujua nani hajaelewa, na maneno 20 ya kumtia moyo anayekosea.
  • Mbinu 5: Kazi za wawili wawili na vikundi vidogo. Kila mwanafunzi aongee, na kila mwanakikundi apewe kazi yake.
  • Mbinu 6: Kitabu kila wiki, kama Ben Carson. Jinsi vitabu viwili vya maktaba kila wiki vilivyomtoa mvulana mkiani mwa darasa hadi kuwa daktari bingwa duniani, na jinsi ya kufanya hivyo darasani au nyumbani.
  • Mpango wa wiki 4 wa kuanza hatua kwa hatua.
  • Sura ya wazazi, yenye mambo 10 ambayo mzazi anaweza kufanya nyumbani.
  • Fomu 10 za kuchapisha: chati ya maendeleo ya darasa, fomu ya kuandaa maswali, fomu ya kuandaa somo la mchezo, kikaratasi cha mwisho wa kipindi, maneno ya kusifu, kadi za kazi za kikundi, daftari la usomaji, ripoti ya kitabu, fomu ya kufuatilia kila mwanafunzi, na maswali ya mwalimu ya kila wiki.

Ni kwa ajili ya nani: walimu wa shule za msingi na sekondari, wazazi na walezi, wakufunzi wa tuisheni, wakuu wa shule, na mashirika yanayoendesha programu za elimu.

Muundo: PDF (kurasa 28 za A4, zenye picha), pamoja na faili la Word (.docx) unaloweza kubadilisha. Pia lipo toleo la Kiingereza: From Struggling to Soaring.

Umeandaliwa na Wellbiz Solutions, Tanzania. Tunaunganisha sayansi ya asili na hekima ya maisha ya kila siku.

You will get the following files:
  • PDF (2MB)
  • DOCX (3MB)
  • DOCX (3MB)