KWA NINI BAADHI YA WATU WANATOA PUMZI YENYE HARUFU MBAYA SANA?!
“KWA NINI BAADHI YA WATU WANATOA PUMZI YENYE HARUFU MBAYA SANA? – Jinsi ya Kujitibu kwa Mafanikio” ni kijitabu cha kidijitali (ebook) cha Kiswahili kinachoelezea kwa urahisi kila kitu unachohitaji kujua kuhusu pumzi mbaya (halitosis) – kuanzia sababu zake, aina mbalimbali za tatizo, hadi hatua sahihi za uchunguzi, matibabu hospitalini na matibabu ya njia ya asili. Kitabu hiki kinafaa kwa mtu yeyote anayeteseka kwa harufu mbaya ya pumzi, anayeshindwa kujiamini mbele ya watu, au mtoa huduma ya afya na hata matabibu wa tiba asili wanaotaka uelewa wa kitaalamu na unaoeleweka kirahisi.
Ndani ya kitabu utajifunza: namna matatizo ya kinywa (meno, fizi, ulimi, ukavu wa kinywa, tumbaku n.k.) yanavyochangia zaidi ya asilimia 80 ya visa vya halitosis, namna magonjwa mengine ya mwili kama matatizo ya tumbo, sinusitis, kisukari, figo na ini yanavyoweza kubadilisha harufu ya pumzi, pamoja na hatua za uchunguzi zinazofanyika hospitalini ili kubaini chanzo halisi cha tatizo. Pia utapata mwongozo wa matibabu ya kitaalamu ya mdomo na meno, tiba za asili zinazoweza kusaidia, pamoja na mbinu muhimu za kila siku za kuboresha usafi wa kinywa, lishe na mtindo wa maisha ili kurejesha pumzi safi na kujiamini katika mahusiano ya kifamilia, kazini na kijamii.

Kijitabu hiki ni cha kupakua mara moja (digital download), na rahisi kusoma kwenye simu, tablet au kompyuta; na unaweza kuyarejea maudhi wakati wowote unapotaka kufuatilia hatua za matibabu au kuwashauri wengine