Your Cart

FURSA3000 ZINAZOKUZUNGUKA AFRIKA MASHARIKI NA MTAJI WA KUANZIA

On Sale
$5.00
$5.00
Added to cart
Mabadiliko makubwa yanayotokea duniani hivi sasa ya kisayansi na kiteknolojia yameleta changamoto nyingi sana katika uchumi wa dunia. Mabadiliko haya pamoja na kwamba yameleta ukuaji mzuri wa uchumi kwa siku za hivi karibuni, bado madhara yake ni bayana na yanahitaji mjadala mpana.

Changamoto hizi ni pamoja na umaskini, njaa na ukosefu wa ajira ndani ya jamii zetu. Hii inatokea pale ambapo shughuli nyingi ambazo zilikuwa zikifanywa na wanadamu kwa muda mrefu, sasa zinafanywa na mashine. Hali hii imepelekea maisha kuwa magumu kiasi cha kufikirisha sana viongozi na watunga sera kuchekecha maarifa yatakayoleta suluhu ya changamoto hizi.

Umoja wa mataifa katika kujaribu kutafuta suluhu wa mambo haya, ulikaa na kubainisha changamoto kumi na saba ambazo lazima zipewe kipaumbele. Nyingi kati ya hizo zinalenga kuleta usawa miongoni mwa wanajamii. Serekali ya Tanzania hali kadhalika imekuja na malengo na sera mbalimbali ili kuweza kupambana na hizi changamoto ikiwa ni pamoja na mipango ya kitaifa ya muda mrefu na muda mfupi. Hizi zote zikiwa ni namna ya kutafuta ufumbuzi wa changamoto hizi.

Fursa3000 imekuja muda mwafaka. Muda ambapo changamoto kubwa ni namna ya kubambana na umaskini, njaa na ajira. Lakini watu wetu wengi wamekata tamaa kwa sababu biashara nyingi zinazoanzishwa hazifiki mbali. Kupata wazo bora la biashara, mitaji ya kuendesha biashara, usimamizi mzuri wa biashara umekuwa changamoto pia. Kitabu cha Fursa3000, tumejikita sana kwenye utoaji wa fursa bora za biashara zinazofaa kwa kila mkoa ndani ya Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Sudan Kusini na Afrika nzima. Lengo likiwa ni kutengeneza nafasi nyingi zaidi za watu kujiajiri kupitia ujasiriamali.

Tunawakaribisha watu wote kupitia kurasa zetu ili kupata taarifa zinazohusu fursa za uwekezaji. MITANDAO YA KIJAMII NI @fursa3000.
You will get a PDF (1MB) file