Your Cart
Loading

Misingi na Mbinu za Kudhibiti Msongo wa Mawazo na Kukuza Mazingatio (Mwongozo + Zana 7)

On Sale
$12.00
$12.00
Added to cart

Msongo wa mawazo ni sehemu ya maisha. Kuelemewa nao si lazima.

Ada za shule, marejesho ya mkopo, michango, kazi isiyoisha na simu isiyonyamaza: wengi wetu tunabeba mzigo mkubwa kuliko mwili unavyoweza kustahimili. Baada ya muda unajitokeza kama kukosa usingizi, kichwa kuuma, hasira za haraka na akili isiyotulia.

Mwongozo huu unakupa misingi na mbinu za kudhibiti msongo: njia rahisi zilizothibitishwa, unazoweza kuanza kuzitumia leo, kwa lugha nyepesi na kwa dakika kumi tu kwa siku.


Utakachojifunza

  • Msongo unavyoathiri mwili na akili, na kwa nini unadhibitika kwa mazoezi
  • Njia tatu za kuutuliza mwili ndani ya dakika chache: kupumua taratibu, kukagua mwili na kulegeza misuli
  • Jinsi ya kuyakamata na kuyahoji mawazo yanayochochea msongo
  • Jinsi ya kumudu hisia kali bila kuzimeza wala kulipuka
  • Jinsi ya kusikiliza na kuzungumza kwa namna inayopunguza migogoro
  • Jinsi ya kupanga muda, kuweka mipaka na kusema hapana kwa adabu
  • Jinsi ya kujenga mazoea ya mazingatio yatakayodumu


Zana 7 zilizomo

  • Kipimo cha msongo, cha kujipima sasa na tena baada ya wiki nne
  • Daftari la fikra
  • Mwongozo wa kukagua mwili kwa dakika kumi
  • Pumziko la dakika tatu
  • Jedwali la haraka na muhimu
  • Mpango wa kuanzia wa siku saba
  • Mpango binafsi wa mazoezi


Ni kwa ajili ya nani

Wafanyakazi, wafanyabiashara, wazazi, wanafunzi na yeyote anayejiona ameelemewa na anataka hatua za vitendo za kufuata. Huhitaji uzoefu wowote wa kutafakari.


Utakachopata

Faili la PDF lenye kurasa 47 na picha, linalosomeka kwenye simu, tableti au kompyuta. Kurasa za zana zinaweza kuchapishwa. Unalipakua mara baada ya kulipa.


Kinapatikana pia kwa Kiingereza: The Bolts and Nuts of Stress Management and Mindfulness Cultivation.

Mwongozo huu ni wa elimu na kujisaidia. Hauchukui nafasi ya huduma ya daktari au mtaalamu wa afya ya akili.

You will get a PDF (3MB) file