Your Cart
Loading

Mdundo wa maneno

On Sale
$3.24
$3.24
Added to cart

Dieudonné Bacinoni ni mwandishi na mshairi mwenye uraia wa Burundi. Alizaliwa tarehe 16 septemba 1969 Ngagara mjini Bujumbura. Zaidi ya miaka ishirini ya ukimbizi nchini Rwanda. Aliekuwa mpiganaji wa kikundi cha CNDD-FDD. Afisa mkuu katika Jeshi la Polisi Burundi. Shahada ya kwanza ya chuo katika Mawasiliano kwa Maendeleo, akikaribia kupata shahada ya pili katika Uongozi na Usimamizi wa Mashirika. Mke na watoto wanne.

 

Kitabu Mdundo wa maneno kinaundwa na mashairi thelathini. Yalitungwa kulingana na kanuni za ushairi wa lugha ya Kifaransa. Lugha ya Kiswahili huongewa na huelewa na Warundi, hususani wakaazi wa miji wanaoshughulika na kazi kadhaa, kama vile wafanyabiashara na madereva. Tena, Burundi ni miongoni mwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki. Mwandishi wa kitabu hiki ana lengo la kufundisha Kiswahili kupitia sanaa ya ushairi na anatoa mdundo unaomsumbua moyoni mwake, akitumia maneno tu bila vifaa vya muziki. Ndipo, mengi ya mashairi yake ni kama nyimbo zinazopendwa na vijana, na hakusahau kushauri watu kujikinga na janga la UKIMWI. Kifupisho hicho hujificha katika baadhi ya mashairi. 


You will get a PDF (1MB) file