Your Cart
Loading

Andika Business Plan Inayoaminika na Benki na Wawekezaji: Mwongozo wa Hatua kwa Hatua + Zana 9

On Sale
$15.00
$15.00
Added to cart

Andika business plan inayoaminika na benki, SACCOS na wawekezaji, hata kama hujawahi kuandika hata moja.

Business plan nyingi hazikataliwi kwa sababu wazo ni baya, bali kwa sababu mpango hauko wazi, una matumaini makubwa mno au unakosa namba ambazo mkopeshaji anahitaji kuziona. Kit hii inakupitisha katika kila sehemu ya mpango imara, hatua kwa hatua. Inafuatilia biashara moja ya Kitanzania, bekari iliyoko Sinza, Dar es Salaam, tangu wazo hadi ombi la mkopo, na inakupa zana zilizo tayari zinazokufanyia hesabu ngumu.

Utakachopata (mwongozo wa kurasa 55 + zana 9)

  • Mwongozo wa PDF wenye michoro (kurasa 55, sura 16): vipengele 13 vya business plan imara kwa mpangilio unaopaswa kuviandika, wakopeshaji na wawekezaji wanaangalia nini ("C tano" za mikopo), makosa 12 yanayoangusha business plan, na mpango wa siku 30 wa kukamilisha yako.
  • Zana 8 za Word zinazoharirika: Kiolezo cha Business Plan (vipengele vyote 13 pamoja na maswali elekezi), Business Plan ya Ukurasa Mmoja, Fomu ya Utafiti wa Soko na Dodoso la Wateja, Fomu ya Uchambuzi wa Washindani na SWOT, Fomu ya Mpango wa Masoko na Mauzo, Kiolezo cha Wasifu wa Timu, Rejista ya Hatari na Mpango wa Dharura, na Orodha ya Ukaguzi wa Mwisho.
  • Kikokotoo cha Fedha cha Excel chenye kurasa 7 zinazounganika: gharama za kuanzia, vyanzo vya fedha na marejesho ya mkopo, dhana za mauzo na gharama, mtiririko wa fedha wa miezi 12, faida na hasara ya miaka 3, uchambuzi wa kurudisha gharama (break-even) na kipimo cha hali nzuri, ya kawaida na mbaya. Kimejazwa mfano ili uone jinsi kinavyofanya kazi kabla ya kuweka takwimu zako.

Utajifunza jinsi ya:

  • Kukadiria soko lako kutoka chini kwenda juu, pamoja na vyanzo ambavyo mkopeshaji anaweza kuvikagua
  • Kukokotoa hasa kiasi cha fedha unachohitaji, ikiwa ni pamoja na akiba ya mtaji wa kuendeshea ambayo wengi husahau
  • Kuthibitisha kwamba mtiririko wako wa fedha unaweza kurejesha mkopo, mwezi kwa mwezi
  • Kupata kiwango chako cha kurudisha gharama na kupima kitakachotokea katika mwezi mbaya
  • Kuandika muhtasari wa kiutekelezaji unaomfanya msomaji mwenye shughuli nyingi aendelee kusoma

Inafaa kwa wajasiriamali wanaoomba mkopo wa benki, SACCOS au taasisi za fedha ndogo, wamiliki wa biashara wanaopanga kupanua, wanaoomba ruzuku, mashindano, zabuni au usajili wa uwekezaji, na washauri wanaoandikia wateja mipango.

Imeandikwa na Juma Killaghai, Mshauri wa Biashara na Mwandishi, Wellbiz Solutions, Dar es Salaam. Inafanya kazi kwenye Microsoft Word na Excel, Google Docs na Sheets, na LibreOffice.

Unapendelea Kiingereza? Toleo la Kiingereza: payhip.com/b/ed3NI

You will get the following files:
  • PDF (2MB)
  • DOCX (20KB)
  • DOCX (12KB)
  • DOCX (14KB)
  • DOCX (13KB)
  • DOCX (13KB)
  • DOCX (13KB)
  • DOCX (13KB)
  • DOCX (14KB)
  • XLSX (26KB)