Your Cart

FURSA, ANZIA SOKONI

On Sale
$3.00
$3.00
Added to cart
Preview
Duniani kuna fursa za kutengeneza pesa kwa haraka na fursa zinazotengeneza pesa kwa muda mrefu. Kuna fursa za kutengeneza pesa kidogo na fursa za kutengeneza pesa nyingi. Kuna fursa za kutajirisha watu na fursa zenye kuleta hasara. Kuna fursa za tangu enzi na enzi na fursa mpya. Kuna fursa za kukunufaisha wewe na za kuwanufaisha watoto na wajukuu wako.

Sasa utafanyaje ili upate kuchagua fursa nzuri ya kufanya? Ni lipi wazo zuri la biashara la kufanyia kazi? Ni lipi wazo dogo la biashara la kufanya nyumbani kwa fedha kidogo? Ni lipi wazo la biashara lenye uwezekano wa kukua kwa haraka na kutengeneza pesa za kutosha kwa muda mfupi?
Utajuaje kama fursa niliyochagua itakulipa vyema? Je, uliwahi kuwaza kumiliki biashara yako wenyewe? Je, kuna haja ya wewe kuwa tajiri na kumiliki biashara kubwa yenye kuajiri mamia ya watu? Je, unapesa na nia ya kuanziasha biashara yako lakini umeshindwa kufanya maamuzi juu ya biashara sahihi ya kufanya? Kama haya maswali yote yanaelezea hali uliyonayo, basi nakusihi utenge muda wa kutosha ili upitie kitabu hiki mwanzo hadi mwisho.

Wajasiriamali wengi huchanganyikiwa pale wanapotaka kuanzisha biashara kwani hushindwa kujua fursa sahihi ya kufanyia kazi. Mimi mwenyewe nikiwa bado nipo chuoni nilipokea simu kutoka kwa marafiki zangu zaidi ya watano hivi, mmoja ambaye tayari alikwishahitimu chuo kikuu na ameajiriwa. Aliniuliza hivi;
“Nashon habari za siku? Wewe nakufahamu ni mzee wa fursa tangu tupo chuoni ulikuwa unapenda sana mambo ya fursa fursa hivi. Mwenzio ninataka kuanzisha biashara naomba ushauri….nina kama milioni sita hivi…”

Jibu la moja kwa moja kwa swali kama hili laweza kuwa gumu kidogo. Nilitamani nikae naye kwenye somo hili la ujasiriamali kwa walau muda fulani kisha achague mwenyewe. Pamoja na kuwa nilimpa chaguo nililoliona linamfaa kulingana na ninavyomjua, bado ninahisi nilifanya kosa kubwa. Kosa hilo sitaki kulirudia kwako wewe unayesoma kitabu hiki leo.
Chamsingi, wewe fuatilia kitabu hiki kuanzia mwanzo mpaka mwisho bila kuruka kurasa. Usisome sehemu moja tu ukakimbia na kuanza biashara kabla ujamaliza kitabu. Ukifanya hivyo utagundua kuna biashara fulani ndio bora na utaanza tena fursa nyingine upya mwisho wa siku ni kuchanganyikiwa na kuona kuwa kitabu hakijakusaidia.

Vitabu vingi sana vimeandikwa kuhusu ujasiliamali. Je, unajua utofauti uliopo kati ya vitabu hivyo na hiki? Vitabu vingi vinatoa ushauri tu. Utasikia fanya kazi sana, jitume, acha uzembe, kuwa mbahiri, amka alfajiri fanya kazi yoyote ile! Hakuna mtu aliyewahi kufanya kazi yoyote akafanikiwa! Lazima kazi unayoifanya uijue ndipo uifanye kwa ustadi mkubwa. Mfano, mimi nimeandika kitabu hiki, kwahiyo, hii ni kazi yoyote? Swali ni kwamba, mtu afanye kazi gani? Hawana majibu, utasikia kazi yoyote ili mradi mkono uende kinywani. Kosa! Ifikie hatua tuwape watu orodha ya fursa na mchanganuo wa mtaji wa kuanzia ili wao wenyewe wachague cha kufanya.

Pamoja na hayo, ili mtu awe mjasiriamali hodari haitegemei fursa zilizopo tu, inategemeana na yeye mwenyewe kwa kiasi kikubwa. Kama unataka kuwa mjasiriamali hodari lazima ujitambue kweli kweli na uchague wazo linalokufaa. Usifanye kwa kuwa fulani kafanya, fanya kwa kuwa wewe mweyewe unauwezo wa kumudu fursa husika. Mfano, mimi ukiniambia niimbe kama Michael Jackson, siwezi! Lakini ukiniambia niandike kitabu kuhusu ninavyomjua

Michael Jackson naweza kuandika vizuri. Hivyo pamoja na kuwa zipo fursa zinazoweza kufanywa na kila mtu, kuna fursa zingine ambazo zinalenga watu falani fulani katika jamii. Mfano mwingine, fursa ya kucheza mpira wa miguu. Fursa hii moja kwa moja inamlenga kijana wa kati ya miaka 14-30 kwa mtu mwenye miaka 50 hawezi na hivyo itamlazimu kuchangua fursa nyingine.

Endapo msomaji hataelewa fursa fulani vizuri, asisite kuwasiliana nasi kwa namba za simu na mitandao ya kijamii kama ilivyoorodheshwa kwenye kurasa ya mwisho wa kitabu hiki. Ahsante.
You will get a PDF (2MB) file